19 Machi 2011 - 20:30

Spika wa bunge la taifa la Sudan ameiomba jamii ya kimataifa isaidie kuboresha uchumi wa nchi hiyo. Ahmad Ibrahim at- Tahir spika wa bunge la taifa la Sudan ameiomba jamii ya kimataifa iisaidie Sudan ili iweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi baada ya kujitenga na Sudan Kusini

Spika wa bunge la taifa la Sudan ameiomba jamii ya kimataifa isaidie kuboresha uchumi wa nchi hiyo. Ahmad Ibrahim at- Tahir spika wa bunge la taifa la Sudan ameiomba jamii ya kimataifa iisaidie Sudan ili iweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi baada ya kujitenga na Sudan Kusini. Ahmad at-Tahir ambaye yuko ziarani nchini Norway katika fremu ya safari zake za kiduru barani Ulaya amesema kuwa Sudan imepoteza sehemu ya mapato yake ya mafuta na kwamba serikali ya Khartoum inafanya juhudi kutatua matatizo yake ya kiuchumi kwa kuomba msaada kutoka nchi rafiki na kwa kutumia suhula ilizonazo. Spika wa bunge la taifa la Sudan amesisitiza juu ya azma ya nchi hiyo ya kupambana na ugaidi na kukabiliana na njama yoyote inayotishia usalama wa raia wa nchi hiyo. Ameongeza kuwa Khartoum inafanya kila iwezalo ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliyoko katika maeneo ya mpakani baina yake na Sudan Kusini.